KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, May 19, 2011

FC PORTO MABINGWA EUROPA LEAGUE 2010-11.Baada ya kutwaa ubingwa wa kombe la ligi ya barani ulaya *EUROPA LEAGUE* meneja wa klabu ya FC Porto Andre Villas-Boas amesema walikua hawana budi kupata taji la michuano hiyo kufautia juhudi walizozionyesha toka walipoanza kampeni hiyo katika mzunguuko wa tatu.

Andre Villas-Boas alieweka rekodi ya kuwa meneja mwenye umri mdogo aliefanikiwa kutwaa ubingwa michuano ya kombe la barani Ulaya pamoja na ubingwa wa ligi ya nchini Ureno amesema kiujumla wachezaji wake walionyesha hamu ya kutafuta mafanikio katika michuano hiyo na mwisho wa siku wamefanikiwa na suala hilo linaendelea kujidhihirisha wazi.

Andre Villas-Boas kwa sasa ana umri wa miaka 33 na kabla ya kuweka rekodi hiyo, Jose Mourinho ambae kwa sasa nakinoa kikosi cha Real Madrid alikua kinara katika rikodi hiyo baada ya kuiwezesha FC porto kutwaa ubingwa wa michuiano ya kombe la UEFA *EUROPA LEAGUE* mwaka 2003 akiwa na umri wa miaka 40.

FC Porto wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kufuatia ushindi wa bao moja wka sifuri walioupaya mbele na FC Braga huku bao likifungwa na mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Colombia Radamel Falcao García Zárate.

No comments:

Post a Comment