KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, May 20, 2011

Gervinho AWANIWA NA KLABU ZA NCHINI UINGEREZA.


Klabu ya Arsenal pamoja na Manchester City zimetajwa kupigana vikumbo katika harakati za kumsajili winga wa kimataifa toka nchini Ivory Coast pamoja na klabu inayotarajiwa kutwaa ubingwa nchini Ufaransa Lille Gervais Yao Gervinho.

Klabu ya Arsenal pamoja na Manchester City zimetajwa kuwa katika mbio hizo kufuatia mawakala wa kusaka wachezaji wa klabu hizo mbili kumfuatilia kwa ukaribu sana winga huyo ambae amekua chachu ya kuiwezesha Lille kutarajia kutwaa ubingwa wa nchini Ufaransa msimu huu.

Mbali na klabu hizo kuwa mstari wa mbele kutaka kumsajili Gervais Yao Gervinho, pia imeripotiwa kuwa wakala wa kusaka wachezaji wa klabu ya Tottenham Hotspurs nae amekua akionekekana katika michezo ya hivi karibuni inayoihusu klabu ya Lille kwa ajili ya kumfuatili mchezaji huyo.

Hata hivyo Arsenel pamoja na Man city ndio klabu zinazotajwa sana katika harakati za kumuwania Gervais Yao Gervinho mwenye umri wa miaka 23 ambae pia mkataba wake na klabu ya Lille umesaliwa na mwaka mmoja.

Uongozi wa klabu ya Lille tayari umeshatangaza dau la paund million 9 ambalo litatumika kama ada ya uhamisho wa mchezaji huyo ambae mpaka sasa amshaitumikia klabu hiyo katika michezo 54 na kufunga mabao 25.

No comments:

Post a Comment