KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, May 20, 2011

Hamit Altintop AJIUNGA NA REAL MADRID.


Klabu ya Real Madrid imefanikiwa kumsajili mchezaji wa pili katika kipindi hiki cha kuelekea ukingoni mwa msimu wa mwaka 2010-11 baada ya kukamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa toka nchini Uturuki pamoja na klabu bingwa nchini Ujerumani Borussia Dortmund Nuri Kâzım Şahin majuma mawili yaliyopita.

Mchezaji wa pili aliesajiliwa klabuni hapo ni Hamit Altintop ambae pia anatokea nchini Uturuki na klabu ya have Bayern Munich ya nchini Ujerumania ambayo msimu huu imemaliza ligi ya nchini humo ikiwa katika nafasi ya tatu.

Hamit Altintop mwenye umri wa miaka 28, amejiunga na The Merrengues kwa makubaliano ya mkataba wa miaka minne ambao utamuweka huko Estadio Stantiago Bernabeu hadi mwaka 2015 ambapo sasa anajiunga na wachezaji wengine waliotoka nchini Ujerumani kama Mesut Ozil, Nuri Sahin pamoja na Sami Khedira.

Kiungo huyo ameondoka nchini Ujerumani huku akiacha kumbu kumbu nzuri ya kuwa miongoni mwa wachezaji walioiwezesha Bayern Munich kutwaa ubingwa wa ligi katika msimu wa mwaka 2007-08, kombe la nchini Ujerumani mwaka 2010, German Super Cup mwaka 2010 pamoja na kombe la ligi ya nchini Ujerumani mwaka 2007.

No comments:

Post a Comment