KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, May 19, 2011

Khaldoon al-Mubarak APINGA SERA ZA ROBERTO MANCINI.

Mwenyekiti wa klabu ya Manchester City Khaldoon al-Mubarak amehoji utaratibu wa usajili unaotarajiwa kuwasilishwa mezani kwake na meneja wa klabu hiyo Roberto Mancini ikiwa ni sehemu ya mipango ya msimu ujao ambao utashuhudia wakishiriki kwa mara ya kwanza katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Khaldoon al-Mubarak amehoji mpango huo huku akisadiki kwamba haoni sababu ya klabu hiyo kuendelea kutumiza pesa katika usajili wa wachezaji ili hali kikosi kilichopo kina uwezo mkubwa wa kiushindani.

Amesema taarifa za mipango ya meneja huyo kutaka kuongeza mchezaji mmoja kati ya kiungo wa klabu ya Barcelona Xavi Harnandez ama mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo, nae amekua akizisikia kupitia vyombo vya habari lakini anatarajia kuwasilishiwa mezani kwake ila bado akaendelea kuhoji kwa nini usajili huo ufikiriwe?

Amesema kwa sasa huko City of Manchester kuna msingi mzuri wa kuwaendeleza wachezaji waliopo pamoja na kuwanyanyua wale walio katika timu za vijana hivyo bado hajaona ulazima wa kufanya usajili wa wachezaji wenye majina makubwa ulimwenguni ambao wataendelea kuigharimu klabu hiyo iliyo chini ya Taikun wa kiarabu Sheikh Mansour ambae tayari ameshatumia paund bilion moja toka alipoinunua Man City kutoka mikononi mwa aliekua waziri mkuu wa zamani wa Thailand Thaksin Shinawatra.

Miongoni mwa fedha hizo, paund million 350 zilitumika katika usajiali wa wachezaji na sehemu nyingine ya fedha iliyosalia imetumika katika masuala mengine ya kuiendesha klabu hiyo ikiwa sambamba na kulipa mishahara ya waajiriwa.

No comments:

Post a Comment