KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, May 23, 2011

HATIMAE YAMETIMIA KWA CARLO ANCELOTTI.


Meneja wa kimataifa toka nchini Italia, Carlo Ancelotti ametupiwa virago vyake huko Stamford Bridge baada ya kushindwa kufikia malengo yaliowekwa na uongozi wa klabu hiyo ya magharibi mwa jijini London mwanzoni mwa msimu huu.

Ancelotti ametupiwa virago vyake jana usiku ikiwa ni saa kadhaa baada ya kikosi chake kukubali kisago cha bao moja kwa sifuri kutoka kwa Everton waliokua nyumbani huko Goodson Park.

Taarifa rasmi iliyochapishwa kwenye mtandao wa klabu ay Chelsea imeeleza kwamba Ancelotti ametimuliwa kazi kufuatai matokeo mabovu yaliyokiandama kikosi chake mwishoni mwa mwaka jana hatua ambayo ilipelekea klabu hiyo kupoteza muelekeo wa kutetea ubingwa.

Pia taarifa hiyo imedai kwamba mbali na kupoteza muelekea wa kutetea ubingwa wa nchini Uingereza, meneja huyo alishindwa kukiwezesha kikosi chake kufanya vyema katika michuano mingine waliyoshiriki ikiwa ni pamoja na michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Kufuatia maamuzi hayo, Ancelotti anakua meneja wa tatu kutimuliwa kazi klabuni hapo, baada ya kadhia hiyo kumkuta Jose Mourinho mwaka 2007, Luiz Felipe Scolari pamoja na Avram Grant mwaka 2008.

Mameneja wanaotajwa kuchukua nafasi ya Carlo Ancelotti huko Stamford Bridge ni kocha wa timu ya taifa ya Uturuki Gus Hidink pamoja na meneja wa klabu ya FC Porto Andre Villas Boas.

No comments:

Post a Comment