KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, May 23, 2011

MLENGWA NA MAN UTD AWA MCHEZAJI BORA UFARANSA.


Kiungo wa kimataifa toka nchini Ubelgiji pamoja na Lille Eden Hazard ametajwa kuwa mchezaji bora wa ligi daraja la kwanza ya nchini humo kwa msimu wa mwaka 2010-11.
Eden Hazard ambae amekua mstari wa mbele kuhakikisha Lille wanatwaa ubingwa wa ligi ya nchini Ufaransa msimu huu, hatau mbayo imefanikiwa, ametajwa kushika nafasi hiyo kutokana na umahiri wake aliouonyesha akiwa uwanjani.

Mbali na kuiwezesha Lille kutwaa ubingwa wa ligi pia kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 amebebwa na sifa nyingine ya kupigana kufa na kupona na kuiwezesha klabu yake kutwaa ubingwa wa kombe la nchini ufaransa.

Katika hatua nyingine meneja wa klabu ya Lille Rudi Garcia ametajwa kuwa meneja bora wa nchini Ufaransa katika msimu wa mwaka 2010-11.

Katika hatua nyingine kikosi cha wachezaji 11 bora kilichotokana na umahiri wa wachezaji walioshiriki ligi ya nchini ufaransa nacho kimetajwa ambapo:

Steve Mandanda (Olympique Marseille) - Anthony Reveillere (Olympique Lyon), Adil Rami (Lille), Mamadou Sakho (Paris St Germain), Taye Taiwo (Olympique Marseille) - Yann Mvila (Stade Rennes), Gervinho (Lille), Eden Hazard (Lille), Nene (Paris St Germain) - Kevin Gameiro (Lorient) pamoja na Moussa Sow (Lille).

No comments:

Post a Comment