KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, May 26, 2011

NINI HATMA YA Alberto Aquilani KURUDI LIVERPOOL AMA KUBAKI JUVE?


Hatma ya kiungo wa kimataifa toka nchini Italia Alberto Aquilani ya kurejea kwenye klabu yake ya Liverpool kwa ajili ya msimu ujao akitokea Juventus alipopelekwa kwa mkopo itafahamika juma lijalo kama anabaki huko Stadio Olimpico di Torino ama la.

Wakala wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 amelazimika kulizungumza suala hilo kufuatia fununu zinzoendelea miongoni mwa waandishi wa habari ambapo wamekua wakitangaza na kuandika kwamba Alberto Aquilani hana budi kurejea jijini Liverpool baada ya uongozi wa klabu ya Juventus kumsajili Adrea Pirlo kwa makubaliano ya mkataba wa miaka mitatu.

Franco Zavaglia wakala wa mchezaji huyo amesema kwa sasa bado wanatafuta namna ya kuzungumza na viongozi wa klabu ya Liverpool kwa ajili ya kutafuta suluhu ya kumrejesha mchezaji huyo ama kumuuza moja kwa moja ili aweze kurejea nyumbani.

Wakati huo huo uongozi wa Juventus umeendelea na harakati za kukisuka upya kikosi chao kufuatia kukamilisha taratibu za kumsajili mshambuliaji wa pembeni kutoka nchini Uswiz Reto Ziegler.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, amesajiliwa huko Stadio Olimpico di Torino, kwa uhamisho huru akitokea kwenye klabu ya Sampdoria ambayo msimu ujao itacheza ligi daraja la kwanza nchini Italia.

No comments:

Post a Comment