KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 31, 2011

Johan Elmander AJIUNGA NA Galatasaray ya nchini Uturuki


Hatimea aliekua mshambuliaji wa klabu ya Bolton Wanderers Johan Elmander amekamilisha taratibu za kujiunga na klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amekamilisha utaratibu huo huku akisaini mkataba wa miaka mitatu wa kuichezea klabu hiyo ya Türk Telekom Arena.

Johan Elmander amekamilisha utaratibu huo baada ya kuondoka Reebok Stadium, alipogoma kusaini mkataba mpya hatua ambayo ilimfanya kuondoka mwishoni mwa msimu wa mwaka 2010-11 akiwa kama mchezaji huru.

Kusajiliwa kwa Johan Elmander kunaifanya klabu ya Galatasaray kufikisha idadi ya wachezaji sita waliowasajili katika kipindi hiki kwa ajili ya msimu ujao wa ligi ambapo miongoni mwa wachezaji hao yupo Jlloyd Samuel, Joey O'Brien, Tamir Cohen, Sam Sheridan, Maison McGeechan pamoja na Tom Eckersley.

No comments:

Post a Comment