KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, May 20, 2011

Johan Elmander KUITEMA BOLTON WANDERERS BAADA YA J2.Meneja wa klabu ya Bolton Wanderers Owen Coyle anategemea mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Sweden pamoja na klabu hiyo Johan Elmander ataondoka klabuni hapo na kujiunga na klabu ya Galatasaray ya nchini Uturuki kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Elmander, mwenye umri wa miaka 29, anafikiriwa huenda atajiunga na klabu hiyo kufuatai kugoma kusiani mkataba mpya na uongozi wa klabu ya Bolton Wanderers huku mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kufikia kikomo mara baada ya mchezo wa mwishoni mwa msimu huu ambao utapigwa huko Reebok Stadium dhidi ya Manchester City siku ya juma pili.


Owen Coyle imemelazimu kuzungumza taarifa za mshambuliaji huyo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika hii leo huko Reebok Stadium ambapo alikua akimtakia kila la kheri huko aendako baada ya kufanya kazi nzuri msimu huu ya kusaidiana na wengine klabuni hapo katika michuano yote waliyoshiriki.

Amesema ataukumbuka sana mchango wa mshambuliaji huyo lakini hana budi kuanza kuyazoea mazingira ya kumkosa kikosini kuanzia msimu ujao ambao ameutabiria utakua mgumu kwa kila klabu itakayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

Owen Coyle amesema uongozi wa klabu ya Galatasaray tayari umeshatangaza nia ya kutaka kumsajili Johan Elmander kupitia mtandao wa klabu hiyo na anaamini kila jambo litakaa sawa ndani ya majuma kadhaa yajao.


Wakati Johan Elmander akiwa mbioni kuondoka huko Reebok Stadium, winga wa kimataifa toka nchini Uingereza pamoja na klabu ya Aston Villa Ashley Young,ameshindwa kuthibitisha wazi mustakabali wa maisha yake huko Villa Park huku kidai kwamba kwa sasa anaupa nafasi kubwa mchezo wa mwisho wa ligi utakaochezwa siku ya jumapili dhidi ya Liverpool.

Ashely Young amesema kwa sasa ni vigumu kueleza wazi mustakabali wake zaidi ya kusubiri msimu ufikie kikomo siku ya jumapili, na baada ya hapo itaeleweka ni wapi anaelekea ama kubaki ndani ya klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment