KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, May 20, 2011

Luigi De Canio AWAPUNGIA MKONO WATU WA LECCE.


Meneja wa klabu ya Lecce Luigi De Canio imethibitisha atafungasha virago vyake mara baada ya mchezo wa mwisho wa ligi utakaochezwa siku ya jumapili dhidi ya SS Lazio katika uwanja wa Via del Mare.

Luigi De Canio mwenye umri wa miaka 53 anaondoka klabuni hapo kwa sababu zake binafsi na pia ameutakia kheri zote uongozi wa klabu ya Lecce ambao ulimpa majukumu ya kukiendesha kikosi chao toka mwaka 2009 na kufanikiwa kukirejesha katika ligi kuu nchini humo msimu huu.

Amesema ni maamuzi mazito anayoyachukua lakini hana budi kufanya hivyo kwa lengo la kumpisha meneja mwingine aendeleze mazuri aliyoyafanya ambapo anaamini hakuna kitakacho shindikana.

De Canio, mara baada ya kuiwezesha Lecce kurejea ligi kuu msimu huu amejitahidi kuinusuru klabu hiyo kutokurejea tena katika ligi daraja la kwanza baada ya kikosi chake kupata point za kutosha ambazo zinawabakisha katika ligi ya Sirie A kwa ajili ya msimu ujao.

No comments:

Post a Comment