KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 24, 2011

Ryan Giggs NDANI YA KASHFA NZITO.


Winga wa kimataifa toka nchini Wales Ryan Giggs amekosa sehemu ya mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Fc Barcelona utakaochezwa mwishoni mwa juma hili huko jijini London katika uwanja wa Wembley.

Ryan Giggs amekosa sehemu ya mazoezi, ikiwa ni siku moja baada ya kuthibitika wazi kwamba alikua na mahusiano ya kimapenzi na kimada ambae alikua hana ruhusa ya kumtaja kufuatia sheria kumbana za kutokufanya hivyo.

Sababu za kukosa sehemu ya mazoezi ya hii leo kwa winga huyo bado hazijaelezwa wazi lakini inasadikika kwamba huenda aliwahofia waandishi wa habari wasimpige picha kufuatia skendo inayomuandama kwa sasa.

Sakata la kubainika kwa Ryan Giggs kama alikua na mhusiano ya kimapenzi na msichana anaeitwa Imogen Thomas alieshiriki shindano ya BIG BROTHER la nchini Uingereza msimu uliopita limeibukuliwa na na mmoja wa wabunge wa nchini humo aitwae John Hammy ambae alitaka sheria ya kuficha jina la mtu maarufu ama muhimu iondolewe.

Hata hivyo Ryan Giggs si, mchezaji pekee aliekosa mazoezi ya hii leo kwani wachezaji kama Rafael Da Silva, Paul Scholes, Edwin van der Sar pamoja na Dimitar Berbatov walikua katika hali kama hiyo na bado sababu hazijaelezwa wazi.

Waandishi wa habari wasiopungua 200, walionekana katika uwanja wa mazoezi wa Man utd hatua ambayo si ya kawaida na inahisiwa orodha hiyo iliongfezeka kwa lengo la kusaka picha za Giggs.

No comments:

Post a Comment