KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, May 23, 2011

Stuart Pearce APATA PIGO !!!Hatimae kiungo wa kimataifa toka nchini Uingereza pamoja na klabu ay Arsenal Jack Wilshere ametangaza kujiondoa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza chini ya umri wa miaka 21 ambacho mwezi ujao kitaanza kampeni ya kusaka ubingwa wa barani ulaya katika fainali zitakazochezwa huko nchini Denmark.

Jack Wilshere amefikia maamuzi hayo baada ya kufanya mazungumzo na kocha wa timu ya taifa ya vijana ya nchini Uingereza Stuart Pearce, ambapo amemueleza kwamba katika kipindi hiki anahitaji kupumzika baada ya shuruba za ligi kuu kumalizika hapo jana.


Kabla ya maamuzi hayo kufikiwa na kiungo huyo tayari alikua ameshajumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza hatua ambayo ilipingwa vikali na meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger kwa kuidai kwamba Jack Wilshere anahitaji muda wa kupumzishwa.

Mchezaji mwingine alietangaza kujiondoa katika timu ya taifa ya vijana ya nchini Uingereza chini ya umri wa miaka 21 ni mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Andy Carroll ambae pia ameomba kupumzishwa baada ya kash kash za ligi kuu.

No comments:

Post a Comment