
Beki wa kimataifa toka nchini Ivory Coast, Abdoulaye Meite amekubalia kiujiunga na klabu ya Dijon ya nchini ufaransa ambayo itashiriki michuano ya ligi daraja la kwanza nchini humo msimu ujao.
Abdoulaye Meite amekubali kujiunga na klabu hiyo, akitokea nchini Uingereza alipokua akiitumikia West Bromwich Albion ambayo imemaliza nae mkataba mwishoni mwa msimu uliopita.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 30 amesaini mkataba wa miaka mitatu na anaaminiwa kuleta changamoto tofauti katika kikosi cha klabu ya Dijon ambacho kitakua kikishiriki ligi daraja la kwanza nchini ufaransa kwa mara ya kwanza.
Abdoulaye Meite ambae tayari ameshaitumikiwa timu ya taifa ya Ivory Coast michezo 48, akiwa barani ulaya toka mwaka 1998, amecheza katika vilabu vitatu tofauti mpaka sasa ambapo mwaka 1998-2000- Red Star Belgrade, mwaka 2000-2006 - Olympic Marseille, mwaka 2006-2008 – Bolton Wanderers na mwaka 2008-2011 West Bromwicha Albion.
No comments:
Post a Comment