KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 30, 2011

CONGO WATUPWA NJE KOMBE LA DUNIA.


Ndoto za timu ya taifa ya Congo Brazzville za kutwaa ubingwa wa dunia chini ya umri wa miaka 17, zimeyeyuka baada ya timu hiyo kukubakia kisago cha mabao mawili kwa moja kilichotolewa na timu ya taifa ya Mexico.

Timu ya taifa ya Congo Brazzaville, *The Baby Red Devils* ilionyesha kuwa tayari kutimiza ndoto hizo baada ya kufanikiwa kutinga katika hatua ya 16 bora, ikitokea katika kundi la kwanza ambalo lishuhudia timu hiyo ikipenya kufuatia kujikusanyia point 4.

Katika mchezo huo wa hatua ya 16 bora Congo Brazzaville waliokuwa wa kwanza kupata bao kwenye dakika ya 53 kupitia kwa Hardy Binguila, lakini dakika 12 baadae Maximiliano Moreira aliifungua Uruguay bao la kusawazisha huku Gaston Silva akipachika msumari wa pili na wa ushindi dakika nne kabla ya kipyenga cha mwisho hakijapulizwa.

Kwa matokeo hayo sasa timu ya taifa ya Uruguay itakutana na timu ya taifa ya Uzbekistan katika hatua ya robo fainali.

No comments:

Post a Comment