
Meneja mpya wa klabu ya Chelsea Andre Villas-Boas amezipuuza taarifa za kiungo wa klabu hiyo kutoka nchini Ghana, Michael Essien kuwa mbioni kuuzwa huko Stamford Bridge.
Andre Villas-Boas ameziopuuza taarifa hizo alipoulizwa na baadhi ya waandishi wa habari ambao walitaka kufahamu ni kweli ana mipango ya kutaka kumtumia kiungo huo aliejiunga na klabu ya Chelsea mwaka 2005 akitokea kwa mabingwa wa zamani wa nchini Ufaransa olympic Lyon.
Andre Villas-Boas amesema kiungo huyo yupo katika mipango yake na anashangazwa na taarifa za Michael Essien kuhusishwa na fununu za kutaka kusajili na klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania , AC Milan ya nchini Italia pamoja na Bayern Munich ya nchini ujerumani.
Taarifa zilizopo zinadai kwamba meneja huyo kutoka nchini ureno ana mipango ya kutaka kuwasajili baadhi ya wachezaji wa FC Porto ambao aliwaongoza kutwaa ubingwa wa ligi pamoja na ligi ya barani Ulaya msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment