KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 30, 2011

Alberto Aquilani KURUDI LIVERPOOL.


Kiungo wa kitaliano Alberto Aquilani amesisitiza mpango wa kuwa tayari kurejea katika klabu yake ya Liverpool, baada ya kuitumikia klabu ya Juventus kwa mkopo wa muda mrefu msimu uliopita.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, ameonyesha utayari huo, baada ya purukushani za hapa na pale zilizojitokeza mwishoni mwa msimu uliopita ambapo iliaminiwa huenda klabu ya Juventus ingemsajili moja kwa moja.

Alberto Aquilani amesema mipango yake mikubwa kwa sasa ni kufikiria namna ya kuisaidia klabu yake ya nchini Uingereza baada ya mikakati ya kutaka kubaki nchini kwao Italia kufeli ambapo tayari kuna taarifa zilizdai kwamba mbali na Juventus klabu zingine kama Napoli pamoja na AC Milan, zimekua zikitaka kumsajili.

Hata hivyo amedia kwamba kwa kipindi chote cha msimu wa mwaka 2010-11 alichokitumia akiwa nchini kwao amejifunza mambo mengi katika soka na hatua hiyo inampa nafasi ya kujiamini katika mipango ya kuwania nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha King Kenny Dalglish.

Alberto Aquilani alisajiliwa na Liverpool mwaka 2009 akitokea AS Roma kwa ada ya uhamisho wa paund million 20, chini ya utawala wa aliekua meneja huko Anfiled Rafael Benitez na aliondoka klabuni hapo kwa mkopo mara baada ya kuajiriwa kwa Roy Hodgson mwanzoni mwa msimu wa mwaka 2010-11.

No comments:

Post a Comment