
Mchezaji mkongwe wa klabu bingwa duniani Inter Milan Javier Zanetti, amekua mhezaji wa kwanza kuukubalia ujio wa meneja mpya Gian Piero Gasperini huko Stadio Giuseppe Meazza.
Javier Zanetti, kiungo alieanza kuitumikia klabu hiyo ya mjini Milan toka mwaka 1995 ameukubali ujio wa Gasperini, ikiwa ni siku mbili tu baada ya meneja huyo kuomba ushirikiano kutoka kwa wadau wote wa Inter Milan.
Akiwa mjini Buenos Aires nchini Argentina na kikosi cha timu ya taifa cha nchi hiyo ambacho kinajiandaa na fainali za mataifa ya Amerika ya kusini, Zanetti amesema Gasperini ni chaguao sahihi na ana imani meneja huyo wa kitaliano atafikia mipango iliyowekwa na raisi Massimo Moratti.
Amesema uzoefu na kuijua ligi ya Italia pamoja na kutambua changamoto za michuano ya kimataifa kwa Gasperini kutoatoa mtazamo tofauti kwa kwa mmoja klabuni hapo na mwishowe watafurahia mwishoni mwa msimu ujao.
No comments:
Post a Comment