KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 30, 2011

Thiago Alcantara AKUBALI KUBAKI BARACELONA.


Mabingwa wa soka nchini Hispania pamoja na barani ulaya kwa ujumla FC Barcelona wamefanikiwa kumbakisha kiungo Thiago Alcantara baada ya kumsainisha mkataba mpya ambao utadumu hadi mwezi June mwaka 2015.

Barcelona wamefanikiwa katika suala hilo, kufuatai mvutano mkubwa ulioibuka kati ya viongozi dhidi ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20, ambae alikua tayari kuondoka na kusajiliwa na klabu nyingine kufuatia kuchoshwa na hatua ya kuwekwa benchi kila kukicha.

Kufanikiwa kwa suala hilo, kunatoa nafasi kwa mabingwa hao kuanza mipango ya kumtengeneza Thiago Alcantara, ili aweze kufikia malengo ya kurithi nafasi ya kiungo wa kispaniola Xavi Hernandez ambae mwezi januari atafikisha umri wa miaka 32.

Mwishoni mwa juma lililopita Thiago Alcantara alikua miongoni mwa wachezaji walioiwezesha timu ya taifa ya Hispania kutwaa ubingwa wa barani ulaya chini ya umri wa miaka 21 baada ya kuifunga timu ya taifa ya Uswiz mabao mawili kwa moja.

Mpaka sasa Thiago Alcantara ameshaitumikia Barcelona katika mchezo mmoja wa ligi ambapo mchezo huo ulikua dhidi ya Real Mallorca, na kwa kipindi chote hiki amekua akicheza kwenye kikosi cha Barcelona B.

No comments:

Post a Comment