KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, June 7, 2011

Alexander Doni KUHAMIA UINGEREZA?


Imethibitika kwamba majogoo wa jiji Liverpool wapo katika mazungumzo ya kutaka kumsajili kipa wa klabu ya AS Roma ya nchini italia Alexander Doni.

Wakala wa kipa huyo kutoka nchini Brazil, Ovidio Colucci amepasua siri hiyo baada ya kuzungumza na uongozi wa klabu ya AS Roma juu ya mustakabali wa mchezaji wake ambae bado ana mkataba huko Stadio Olimpico mjini Roma.

Amesema uongozi wa klabu ya As Roma upo tayari kumuuza kipa huyo endapo mazungumzo kati ya pande hizo mbili yatakwenda kama yalivyopangwa.

Hata hivyo amedai kwamba endapo mazungumzo hayo yatakamilika uongozi wa klabu ya Liverpool bado utakua na shughuli pevu ya kuzungumza na Alexander Doni kwa ajili ya kukubaliana masuala ya maslahi pindi atakapokua huko Mecceyside.

Kipa huyo mwenye umri wamika 31 alijiunga na klabu ya As Roma mwaka 2005 akitokea nchini kwao Brazil kwenye klabu ya Juventude.

No comments:

Post a Comment