KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, June 3, 2011

Andre Dede Ayew AACHWA KIKOSINI.


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ghana Goran Pravi Stevanovic amemtema mshambuliaji wa klabu ya Olympique de Marseille ya nchini Ufaransa Andre Dede Ayew katika kikosi chake kitakachoanza baadae hii leo dhidi ya timu ya taifa ya Congo Brazzaville.

Maamuzi ya kocha huyo ya kumuanzisha bechi Andre Dede Ayew yamewashangaza wengi nchini Ghana kufuatia uwezo wa mshambuliaji huyo hasa ikizingatiwa ametoka kwenye klabu yake ambayo msimu huu aliisaidia kufunga mabao muhimu.

Mshambuliaji huyo inahisiwa ameachwa katika kikosi cha Ghana kufautia mfumo ambao huenda ukatumiwa na kocha huyo katika mchezo wa hii leo kesho dhidi ya Congo Brazzaville ambapo The Black Stars huenda wakacheza kwa mfumo wa 4-2-2-1-1.

Katika kikosi kitakachoanza lipo jina la kiungo wa klabu ya AC Milan ya nchini italia Kevin Prince Boateng ambae atakuwa akicheza kwa mara ya kwanza katika ardhi ya nchini Ghama baada ya kuisaidia timu hiyo kwenye fainali za kombe la dunia huko nchini Afrika kusini mwaka 2010.

Kiungo wa klabu ya Chelsea Michael Essien ambae amerejeshwa baada ya kuwa nje kwa muda wa mwaka mmoja nae amejumuishwa katika kikosi hicho ambapo atacheza sambamba na kiungo wa klabu ya Workaholic Agyemang Badu.

No comments:

Post a Comment