
Bossi mpya wa kikosi cha Chelsea Andre Villas Boas amerejesha dongo kwa meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger kwa kusema klabu hiyo itatumia fedha vyovyote vile itakavyotakikana na wala haitosita kufanya hivyo.
Andre Villa Boas amerejesha dongo hilo, zikiwa zimepita siku saba toka alipotangazwa kuwa meneja mpya wa klabu hiyo ya jijini London, ambapo amesema kikosi kizuri siku zote kimekua kikiundwa na wachezaji wazuri na katu huwezi kuwapata wachezaji wa aina hiyo kama hutotumia fedha.
Amesema lengo kubwa la chelsea ni kusaka mafanikio na kufikia malengo iliyojiwekea na anatambua wapo wengi ambao hawapendezwi na utumiaji wa fedha wa klabu hiyo inayomilikiwa na mfanyabiashara wa kirusi Roman Abramovic akiwemo meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger.

Arsene Wenger alitupa dongo huko Stamford Bridge siku chache baada ya kusajiliwa kwa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Hispania Ferdinando Torres akitokea huko Anfield yalipo makao makuu ya klabu ya Liverpool mwezi januari mwaka huu.
Katika moja ya mikutano na waandishi wa habari meneja huyo wa kifaransa alisema hawezi kutumia paund million 50 kumsajili mchezaji mmoja, zaidi ya kuona kiasi hicho cha fedha kitatumika kama kutupwa jalalani.
No comments:
Post a Comment