
Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ivory Coast Gervinho amesema amebakiza sehemu ndogo ya usajili wake ambao utamtoa nchini ufaransa na kuelekea nchini Uingereza katika jiji la London.
Gervinho ambae alikua miongoni mwa wachezaji walioiwezesha klabu ya Lille kutwaa ubingwa wa nchini Ufaransa msimu uliopita amesema suala la kuihama klabu hiyo na kujiunga na klabu ya Arsenal linakwenda vizuri.
Amesema amekubaki kujiunga na Arsenal kutokana na sera ya klabu hiyo kuwajali sana vijana na amaanini kusajiliwa kwake kutaendeleza mikakati ya kusaka mataji ambayo yamekauka huko Emirates kwa muda wa miaka sita iliyopita.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ameongeza kwamba mashabiki wengi ulimwenguni huenda wakawa wameshutushwa na maamuzi ya kukubali kuitumikia klabu ay Arsena lakini ukweli anaufahamu yeye mwenyewe na pia ataudhihirisha atakapokamilisha kila kitu na kufanikiwa kuvaa jezi ya klabu hiyo.
Endapo dili la usajili wa Gervinho litakamilika siku za hivi karibuni kama inavyotarajiwa, Arsenal itakuwa imefanikisha utaratibu wa kuwasajili wachezaji wawili toka kipindi cha usajili kilipoanza mwezi uliopita.
No comments:
Post a Comment