KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 30, 2011

Carson Yeang ATUHUMIWA KWA UDANGANYIFU.


Mmiliki wa klabu ya Birmingham City iliyoporomoka daraja mwishoni mwa msimu uliopita Carson Yeung amefikishwa mahakamani mjini Hong Kong huko nchini China kwa tuhuma za kujipatia fedha kidanganyifu.

Uchunguzi uliofanywa na jeshi la polisi nchini humo limebaini kwamba Carson Yeung amekua akiendesha sehemu ya makampuni yake na kujipatia fedha kidanganyifu na hivyo imelilazimu jeshi la polisi nchini china kumfikisha mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na idara ya ukaguzi wa mahesabu nchini China, imefahamika kwamba mfanyabiashara huyo wa kimataifa, kwa mwaka wa fedha uliopita amejipatia kiasi cha paund million 57 ambazo zimepatikana kinyume na biashara anayoiendesha.

Hata hivyo Carson Yeung yupo nje kwa dhamana na kesi yake itatajwa tena August 11 mwaka huu.

Kufuatia tuhuma hizo, mtendaji mkuu wa klabu ya Birmingham City Peter Pannu amesema hakuna kilichoathiriwa ndani ya klabu hiyo kufuatia kesi inayomkabili Carson Yeang.

Peter Pannu hii leo alitarajiwa kuelekea mjini Hong Kong kwa ajili ya kukutana na bosi wake na inaaminiwa atakaporejea kutoka huko atakuwa na taarifa zaidi zinazohusiana na sakata hilo la kesi.

Kwa kipindi cha miaka minne ambacho kimeshuhudia Carson Yeung akiwa kama mmiliki wa klabu ya Birmingham City, klabu hiyo imefanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe la ligi msimu uliopita, baada ya kuifunga Arsenal mabao mawili kwa moja katika mchezo wa hatua ya fainali.

Na hasara kubwa aliyoipata ni kushuka daraja kwa klabu hiyo ambayo ilifanikiwa kurejea katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza misimu miwili iliyopita.

No comments:

Post a Comment