KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, June 1, 2011

BLATTER KIKAANGONI PEKEE YAKE.


Raisi wa sasa wa shirikisho la soka ulimwenguni kote Josep Sepp Blatter hii leo anatarajia kutetea nafasi hiyo bila ya kuwa na mpinzani katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mjini Zurich nchini Uswiz.

Blatter anajiandaa kutetea nafasi yake bila ya kuwa na mpinzani, kufautia mpinzani wake Mohamed Bin Hammam kutangaza kujiondoa mwishoni mwa juma lililopita kabla ya kusimamishwa kwa muda na kamati ya maadili ya FIFA kufuatia sakata la utoaji wa rushwa.

Barani Afrika hususan nchini Tanzania pamekua na mawazo tofauti kufuatia hatua ya Blatter kutarajia kuendelea kuliongoza shirikisho la soka ulimwenguni FIFA kwa awamu ya nne mfululizo.

Mashabiki wa soka nchini humo baadhi yao wamempinga na wengine wamemkubali kufuatia mambo mbali mbali ambayo amekua akiyafanya katika utawala wake toka mwaka 1998.

Hata hivyo uchaguzi unafanyika hii leo huko mjini Zurich, huku chama cha soka nchini Uingereza pamoja na kile cha nchini Scotland vikiwa vimewataka viongozi wa FIFA kuahirisha uchaguzi huo kufuatia harufu ya rushwa inayonUka ndani ya shirikisho hilo.

Pia hatua hiyo imeungwa mkono na mwanamfalme wa Uingereza William.

Lakini pamoja na kuwepo kwa shinikizo la kutaka tarehe ya uchaguzi isogezwe mbele katibu mkuu wa FIFA Jorome Valke ameshatangaza hadharani kwamba hatua hiyo haitowezekana na kinachofanyika hivi sasa ni kuendelea na taratibu za suala hilo kama zilizopangwa.

No comments:

Post a Comment