KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, June 28, 2011

Jens Lehmann HANA NAFASI KWETU !!!!


Wana nusu fainali wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa mwaka 2010-09 Schalke 04, amezipinga taarifa za kutaka kumsajili aliewahi kuwa kipa wa klabu hiyo Jens Lehmann, alierejea tena katika ulimwengu wa soka mwanzoni mwa mwaka huu baada ya kustahafu soka mwaka 2010 akiwa na klabu ya VfB Stuttgart.

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Schalke 04 Horst Heldt amekanusha taarifa hizo kwa kusema kwamba bado wanaendelea kumsaka mrithi wa Manuel … aliejiunga na klabu ya Bayern Munich mara baada ya kumalizika kwa msimu ulioipita.

Amesema taarifa za wao kuhuisishwa na mipango ya kutaka kumsajili Jens Lehman wanazisikia lakini bado akaendelea kusisitizia jambo la kutokua na mipango ya kumsajili kipa huyo mwenye umri wa miaka 41.

Hata hivyo Horst Heldt amebainisha kwamba siku za hivi karibuni walifanya mazungumzo Jens Lehmann kwa ajili ya kusaka ushauri ambao utawasaidia namna ya kumpa kipa mwenye viwango wanavyobihitaji.

Historia ya Jens Lehmann yaonyesha kwamba klabu yake ya kwanza kuitumikia ilikua Schalke 04 na hii ilikuwa mwaka 1988–1998 na alifanikiwa kudaka katika michezo 274 na kufunga mabao mawili.

No comments:

Post a Comment