KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, May 31, 2011

UCHAGUZI WA FIFA WASHAURIWA KUSIMAMA.


Chama cha soka nchnini Uingereza kimelitaka shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA kuahirisha uchaguzi mkuu wa raisi uliopangwa kufanyika kesho huko mjini Zurich nchini Uswiz huku raisi wa sasa wa shirikisho hilo Josep Sepp Blatter akisalia pekee yake katika kinyang’nyiro hicho kufuatia mpinzani wake kutoka nchini Qatar Mohamed bin Hammam kujiondoa mwishoni mwa juma lililopita.

Ombi la chama cha soka nchini Uingereza limewasilishwa huko FIFA na mwenyekiti wa chama hicho Daudi Bernstein ambapo amedai kwamba hakuna namna ya kuendelea na uchaguzi huo huku harufu ya rushwa ikishamiri miongoni mwa wajumbe wa kamati kuu.

Pia ombi hilo la Chama cha Soka nchini Uingereza limeitaka FIFA kuunda kamati huru ambayo itafanya kazi kwa uwazi kwa kusudio la kufunua maovu ambayo yamekua yakifanyika nyuma ya pazia na mwisho kujitokeza hadharani kwa aibu.

Hata hivyo tayari katibu mkuu wa FIFA Jorome Valke ameshatangaza mbele ya waandishi wa habari hatua za kuendelea kwa uchaguzi kama zilizopangwa siku za nyuma kufuatia mgombea aliesalia Josep Sepp Blatter aliesalia ulingoni kusafishwa na kamati ya maadili ambayo ilimfanyia mahojiano mwishoni mwa juma lililopita sambamba na Mohamed Bin Hammam pamoja na Jack Warner.

No comments:

Post a Comment