KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, June 6, 2011

Fabio Coentrao APASUA UKWELI.


Beki wa pembeni wa klabu ya Benfica ya nchini Ureno Fabio Coentrao amepasua ukweli kufuatia taarifa zilizopo za kutaka kusajiliwa na klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Fabio Coentrao amepasua ukweli huo kufuatia fununu zilizodumu katika vyombo vya habari kwa kipindi cha majuma kadhaa sasa ambapo imeripotiwa kwamba Real Madrid wapo mbioni kumsajili ikiwa ni sehemu ya kutaka kuboresha kikosi chao ambacho msimu wa mwaka 2010-11 kimeshindwa kutimiza malengo ya kutwaa taji la LA LIGA.

Akihojiwa na kituo cha RTP beki huyo mwenye umri wa miaka 23 amesema ni kweli utaratibu wa kutaka kusajiliwa na klabu hiyo upo na anaamini kwa sasa mazungumzo kati ya viongozi wake pamoja na wale wa Real Madrid yanaendelea vyema.

Amesema endapo dili hilo litakamilika kama ilivyopanga atajihisi mwenye furaha kutokana na ndoto kubwa aliyo nayo ya kutaka kuitumikia klabu hiyo ya Estadio Stantiago Bernabeu ambayo kwa sasa ipo chini ya Jose Mourinho kutoka nchini Ureno.

Hata hivyo tayari uongozi wa klabu ya Benfica umeshatangaza ada ya uhamisho wa Fabio Coentrao kuwa ni paund milion 30 ambayo inaaminiwa itamng’oa huko Estadio da Luz.

No comments:

Post a Comment