KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, June 28, 2011

Gian Piero Gasperini AJIWAHI MAPEMAAAAAAAA.


Meneja mpya wa klabu bingwa duniani Inter Milan Gian Piero Gasperini amewataka viongozi, wachezaji pamoja na mashabiki wa klabu hiyo kumpa ushirikiano wa kutosha kwa ajili ya kuendelea kusaka mafanikio.

Gian Piero Gasperini amewasilisha maombi hayo kwa wahusika, kupitia mkutano na waandishi wa habari ambao ulilenga kutambulishwa kwake, baada ya kutangazwa kuwa meneja wa The Nerazzurri mwishoni mwa juma lililopita.

Amesema endapo umoja na mshikano utadumishwa huko Stadio Giuseppe Meazza kutakua na kila sababu za wao kama Inter Milan kufanya vyema na ikiwezekana kurejesha mataji yaliyowaponyoka msimu wa mwaka 2010-11.

Amesema ana shauku kubwa ya kufanya kazi na kila mmoja klabuni hapo huku akiahidi kukutana na mchezaji mmoja baada ya mwingine mara tu watakaporejea mjini Milan kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi.

Gian Piero Gasperini alitangazwa kuw ameneja wa klabu ya Inter Milan akiwa kama chaguo la pili la klabu hiyo, ambayo ililenga kumpatia ajira kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina Marcelo Bielsa lakini sababu ziliozkua nje ya uwezo ziliharibnu dili hilo.

No comments:

Post a Comment