KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, June 28, 2011

Raphael Varane AELEKEA REAL MADRID.


Wafalme wa soka mjini Madrid Real Madrid wamewapiga bao mabingwa wa soka nchini Uingereza Man Utd, kwa kukamilisha usajili wa beki wa kifaransa Raphael Varane kwa mkataba wa miaka sita.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 18 amekamilisha usajili wake baada ya kufanyiwa vipimo vya afya mara baada ya kuwasili mjini Madrid jana mchana akitokea nchini Ufaransa alipokua akiitumikia klabu ya Lens.

Usajili wa mchezaji huyo ambae aliku akiwindwa kwa udi na uvumba na Man utd umeigharimu kiasi cha Euro million 10 klabu ya Real Madrid ambayo ina kiu ya kutwaa ubingwa wa ligi ya nchini Hispania pamoja na ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Beki huyo anaungana na wachezaji wengine wanaocheza katika safu ya ulinzi huko Estadio Stantiago Bernabeu ambao ni Pepe, Ricardo Carvalho, Raul Albiol pamoja na Ezequiel Garay huku akitimiza idadi ya wachezaji wanne waliosajiliwa na real Madrid katika kipindi hiki.

Wachezaji hao ni viungo kutoka nchini Uturuki Nuri Sahin na Hamit Altintop pamoja na mshambuliaji kutoka nchini Hispania Jose Callejon.

No comments:

Post a Comment