KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, June 3, 2011

Guus Hiddink AKIRI KUCHOSHWA NA HABARI ZA CHELSEA.


Kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo Guus Hiddink ameendelea kukanusha taarifa za kuwa mbioni kurejea Stamford Bridge yalipo makao makuu ya klabu ya Chelsea baada ya kuwa huko kwa kipindi cha muda cha msimu wa mwaka 2008-09.

Hiddink ameendelea kukanusha taarifa hizo huku akidai bado mawazo na fikra zake amezielekea katika timu ya taifa ya Uturuki ambayo kwa sasa inasaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Ulaya za mwaka 2012 zitakazofanyika nchini Ukraine pamoja na Poland.

Akizungumza na waandishi wa habari huko mjini Brussels ambapo hii leo patachezwa kabumbu kati ya timu ya taifa ya Uturuki dhidi ya wenyeji Ubelgiji, kocha huyo wa kidachi amesema kwa sasa hana budi kuachwa huru ili aweze kuzungumzia kikosi chake ambacho kinakamata nafasi ya 3 katika kundi la kwanza lenye timu kama Ujerumani, Azerbaijan, Austria pamoja na Kazakhstan.

Guus Hiddink amekua akihusishwa na taarifa za kutaka kurejea Stamford Bridge kwa kipindi cha majuma mawili sasa baada ya Carlo Michelangelo Anceloti aliekua meneja wa klabu ya Chelsea kutimuliwa kazi saa chache baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment