KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, June 3, 2011

Mark Hughes AACHA KAZI CRAVEN COTTAGE.


Uongozi wa klabu ya Fulham ya nchini Uingereza, umethibitisha taarifa za kuondoka kwa meneja wa kikosi chao Mark Hughes baada ya kufanya kazi kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Uongozi wa klabu hiyo inayoongozwa na taykun wa kiarabu Mohamed Al-Fayed umethibitisha taarifa hizo huku ukikiri kwamba Mark Hughes aliwasilisha barua ya kufanya maamuzi ya kuacha kazi klabuni hapo siku kadhaa zilizopita.

Mark Hughes ameondoka Craven Cottage akiwa amekiongoza kikosi cha Fulham katika michezo 43 ya michuano waliyoshiriki katika msimu wa mwaka 2010-11 na kwa bahati mbaya hakufanikiwa kutwaa ubingwa wa aina yoyote zaidi ya kuwawezesha The Cottagers kumaliza katika nafasi ya 8 katika msimamo wa ligi.

Hata hivyo ameondoka klabuni hapo bila ya kukwaruzana na yoyote yule zaidi ya kufanya maamuzi binafsi lakini pia amekanusha taarifa za kuwa mbioni kujiunga na klabu ya Aston Villa ambayo kwa sasa haina meneja kufuatia Garrard Houllier kutangaza kujiweka pembeni kwa muda.

No comments:

Post a Comment