KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, June 7, 2011

Hassan Shehata AJIVUA GAMBA.


Kocha mwenye mafanikio ya kipekee barani Afrika Hassan Shehata amefanya maamuzi ya kubwaga manyanga katika timu ya taifa ya Misri baada ya kukosa muelekeo wa kutetea ubingwa wa fainali za barani humo za mwaka 2012.

Hassan Shehata amefanya maamuzi ya kubwaga manyanga kwa kuwasilisha barua kwenye ofisi za shirikisho la soka nchini Misri ambayo iliainiasha dhamira yake ya kuacha kazi na muda mchache uliofuata ombi lake lilikubwaliwa na uongozi wa EFA.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 61 amefanya maamuzi ya kuondoka katika kikosi cha timu ya taifa ya Misri bila kushurutishwa na mtu yoyote, hatua ambayo imepokelewa kwa huzuni na baadhi ya mashabiki wa soka nchini humo.

Maamuzi hayo yamefanya na Hassan Shehata ikiwa ni siku moja baada ya kikosi chake kupata matokeo ya sare ya bila kufungana na timu ya taifa ya Afrika kusini ahatua mbayo ilidhihirisha wazi kwamba matumaini ya kutetea ubingwa wa Afrika yamepotea kwa asilimia 98.

Katika utawala wake Hassan Shehata akiwa kama kocha wa timu za taifa za nchini Misri.

WASIFU WA HASSAN SHEHATA.

2001-2003: Alikiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Misri chini ya umri wa miaka 20 na kufanikiwa kukipa ubingwa wa vijana wa Afrika mwaka 2003.

2004: Aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya wakubwa wa Misri.

2006: Alishinda taji la kwanza la barani Afrika katika ardhi ya nyumbani baada ya kuibamiza timu ya taifa Ivory Coast kwa mikwaju ya penati.

2008: Alishinda taji la pili barani Afrika katika fainali zilizofanyika nchini Ghana kwa kuifunga timu ya taifa ya Cameroon.

2009: Alikosa nafasi ya kukipelekea kikosi chake katika fainali za kombe la dunia za mwaka 2010 baada ya kufungwa na Algeria katika mchezo wa hatua ya mtoano uliofanyiak nchini Sudan.

2010: Alishinda taji la tatu barani Afrika katika fainali zilizofanyika nchini Angola kwa kuifunga timu ya taifa ya Ghana.

2011: Ametangaza kuacha kazi baada ya kikosi chake kupoteza muelekeo wa kushiriki fainali za mataifa ya Afrika za mwaka 2012 zilitakazofanyika mwezi januari mwakani nchini Gabon pamoja na Equatorial Guinea.

No comments:

Post a Comment