KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, June 8, 2011

MAN UTD WAWAZIDI KETE ARSENAL !!!Imeelezwa kuwa beki wa klabu ya Blackburn Rovers, Phil Jones kwa hivi sasa yupo huko Old Trafford akifanyiwa vipimo vya afya na hii ni kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha nchini Uingereza SKY SPORTS.

Jones, mwenye umri wa miaka 19, yupo mjini Manchester akifanyiwa utaratibu huo baada ya viongozi wa klabu ya Blackburn Rovers kumuwashia taa za kijani ambazo zinampa nafasi ya kujiunga na mabingwa wa soka nchini Uingereza.

Siku kadhaa zilizopita Blackburn Rovers walitangaza hadharani ada ya uhamisho wa beki huyo kuwa ni paund million 16, hatua ambayo ilifungua milango kwa vilabu kama Man utd pamoja na Arsenal kuanza kupigana vikumbo vya kutaka kumsajili.

Hata hivyo televisheni hiyo imeeleza kwamba jana Phil Jones alikua na mazungumzo ya faragha na meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger baada ya kupewa ruhusa ya kufanya hivyo na viongozi wake lakini cha kushangaza hii leo amemgeuka na kuelekea upande wa pili.

Endapo Phil Jones atakamilisha taratibu za kujiunga na klabu ya Man utd, ataendeleza utaratibu wa kujenga ngome kali ya ulinzi ndani ya klabu hiyo kama ilivyo katika timu ya taifa ya Uingereza chini ya umri wa miaka 21 ambapo hucheza sambamba na Chris Smalling.

Wakati Man utd wakiwa katika utaratibu wa kumsajili Phil Jones Arsenal wametangaza kumsajili beki wa klabu ya Charlton Athletics Carl Jenkinson.

1 comment:

  1. arsenal wanataka wachezaji wa mafungu ndio maana wamepigwa kumbo na man u, ubahili wa wenger ndio unaowafanya wawaangalie wenzao wakibebeba vikombe. poleni watu wa arsenal!!!!. andrea G.

    ReplyDelete