KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, June 13, 2011

Mesut Ozil AITOLEA NJE MANA UTD.


Kiungo wa kimataifa toka nchini Ujerumani pamoja na klabu ya Real Madrid Mesut Ozil amezipotezea taarifa za kutaka kusajiliwa na mabingwa wa soka nchini Uingereza Manchester United.

Mesut Ozil amezipotezea taarifa hizo zlipozungumza na muandishi wa habari wa gazeti la The Marca ambapo alimueleza wazi kwamba hana mpango wowote kwa sasa wa kuondoka katika klabu yake ya Real Madrid ambayo ilimsajili mwanzoni mwa msimu wa mwaka 2010-11 akitokea Werder Bremen ya nchini Ujerumani.

Amesema atakua mchoyo wa fadhila endapo atakubali kuondoka Estadio Santiago Bernabeu katika kipindi hiki, kufuatia deni alilo nalo klabuni hapo la kuhakikisha anasaidiana na wengine kutwaa ubingwa wa soka nchini Hispania ambao kwa misimu kadhaa sasa umepotea katika himaya yao.

Hata hivyo Mesut Ozil amekiri kupendezewa na taarifa za kutaka kusajiliwa na klabu kubwa duniani kama Man utd lakini bado akaendelea na msimamo wake kwa kusema muda wa kufanya maamzui hayo haujatimia.

Akicheza kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha Real Madrid katika msimu wa mwaka 2010-11 Mesut Ozil ameonyesha uwezo mkubwa kufuatia uwezo wake binafsi ambao umepelekea kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa mafanikio ya kutwaa ubingwa wa kombe la Mfalme mbele ya mabingwa wa soka nchini Hispania Fc Barcelona.

No comments:

Post a Comment