KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, June 8, 2011

MODRIC HAUZWI !!!!!!!!!!


Meneja wa klabu ya Tottenham Hotspurs Harry Redknapp amechimba mkwara mzito kwa viongozi wa vilabu vilivyopania kumsajili kiungo wa kimataifa toka nchini Croatia pamoja na klabu hiyo ya jijini London Luca Modric.

Harry Redknapp amechimba mkwara kufuatia kiungo huyo kuhusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa kila kukicha hatua ambayo ameipinga kwa kusema Modric hauzwi kama inavyodhaniwa na wengi.

Amesema ni vigumu kufanya maamuzi hayo katika kipindi hiki ambacho kimeshuhudia kikosi chake kikikomaa kiushindani na endapo atafanya hivyo atakuwa anajirudisha nyuma katika mipango ya kufikia malengo aliyojiwekea huko White Hart Lane.

Moja la klabu zinazotajwa sana kuwa mbioni kumsajili Luca Modric ni mabingwa wa soka nchini Uingereza Man utd ambao yasemekana huenda wakatuma ofa ya paund million 20 katika kipindi hiki kwa ajili ya kutimiza mipango yao.

Luca Modric mwenye umri wa miaka 25 alisajiliwa na klabu ya Spurs mwaka 2008 akitokea nchini kwao Croatia alipokua akiitumikia klabu ya Dinamo Zagreb.

No comments:

Post a Comment