KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, June 8, 2011

UJERUMANI YACHUNGULIA UKRAINE NA POLAND.


Michezo ya hatua ya kwanza ya fainali za mataifa ya Ulaya iliendelea tena jana, ambapo timu ya taifa ya Ujerumani imeonyesha hatua ya kukaribia kutinga kwenye fainali hizo baada ya kuitandika timu ya taifa ya Azerbaijan mabao matatu kwa moja.

Ikicheza ugenini katika mji wa Baku huko nchini Azerbaijan timu ya taifa ya Ujerumani ilifanikiwa kupata ushindi huo kupitia kwa mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich Mario Gomez kiungo wa klabu ya Real Madrid Mesut Ozil pamoja na mshambuliaji wa klabu ya Bayer Leverkusen Andre Schuerrle.

Ushindi huo unaendelea kuipa nafasi timu ya taifa ya Ujerumani kuongoza kundi la kwanza kwa kufikisha point 21 ambazo zinatengeneza tofauti ya point 10 dhidi ya timu ya taifa ya Ubelgiji inayokamata nafasi ya pili katika kundi hilo kwa kuwa na point 11.

Matokeo ya michezo mingine wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Ulaya mwaka 2012 iliyochezwa jana ni pamoja na:

Belarus 2-0 Luxembourg
Bosnia-Hercegovina 2-0 Albania
Faroe Islands 2-0 Estonia
San Marino 0-3 Hungary
Sweden 5-0 Finland

No comments:

Post a Comment