KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, June 8, 2011

MOURINHO YUPO LIKIZO QATAR.


Meneja wa klabu ya Real Madrid José Mourinho ametoa ushauri kwa wajumbe wa shirikisho al soka ulimwenguni kote kufikiria namna ya kubadilisha ratiba ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2022 zitakazofanyika nchini Qatar.

Mourinho ametoa ushauri huo akiwa nchini Qatar alipokwenda kupumzika katika kipindi hiki cha mapumziko baada ya kumalizika kwa ligi mbali mbali barani Ulaya ambapo amesema kwa hali ya hewa iliopo sasa nchini Qatar inadhihirishwa wazi kwamba itakuwa vigumu kwa fainali hizo kuchezwa mwezi June.

Amesema wenyeji kadhaa aliokutana nao akiwa nchini humo wamemueleza kwamba katika kipindi hiki cha mwezi June hali ya joto hufikia hadi nyuzi 40 ambayo anaamini itakuwa ni mtihani mzito kwa wageni wataokwenda nchini Qatar kuzishangilia timu zao za taifa.

Hata hivyo mjadala wa kubadilishwa kwa utaratibu wa kucheza kwa fainali za kombe la dunia za mwaka 2022, tayari umeshafungwa ambapo FIFA pamoja na wahusika kutoka nchini Qatar wameshakubaliana usibadilishwe.

No comments:

Post a Comment