KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, June 2, 2011

NIGERIA WAICHAPA ARGENTINA.


Timu ya taifa ya Nigeria usiku wa kuamkia hii leo imejitengeneza mazingira ya kujiamini zaidi kabla ya kuendelea na kampeni za kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya barani Afrika za mwaka 2012 kwa kucheza na timu ya taifa ya Ethiopia.

Hali hiyo ya kujiamini inatokana na ushindi wa mabao manne kwa moja walioupata dhidi ya timu ya taifa ya Argentina katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika mjini Abuja.

Nigeria iliwachukua muda wa dakika 10 kupata bao la kwanza kupitia kwa kiungo mshambuliaji wa klabu ya UD Almería ya nchini Hispania Kalu Uche ambae pia alipachika msumari wa pili katika dakika ya 39 huku bao la tatu likifungwa na mshambuliaji wa klabu ya Intert Milan ambae msimu uliopita ameitumikia West Ham utd kwa mkopo Victor Obina katika dakika ya 27.

Bao la nne la timu ya taifa ya Nigeria limefungwa na Emmanuel Chinenye Emenike katika dakika ya 52.

Argentina walipata bao la kufutia machoni katika dakika ya 90 kwa njia ya mkwaju wa penati iliyopigwa na mshambuliaji wa Wigan Atheltics ambae sehemu ya msimu uliopita aliimalizia nchini Hispania kwa mkopo kwenye klabu ya Malaga Mauro Boselli.

Argentina, wameutumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya fainali za mataifa ya bara la Amerika ya kusini *COPA AMERICA* ambazo zimepangwa kufanyika nchini kwao kuanzia July mosi – July 24.

No comments:

Post a Comment