KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, June 1, 2011

Richard Kingson ATANGAZA KUSTAHAFU SOKA LA KIMATAIFA.


Uongozi wa chama cha soka nchini Ghana umethibitisha kuwa katika mazungumzo na kipa tegemezi wa timu ya taifa ya nchi hiyo Richard Kingson ambae amepanga kustahafu soka la kimataifa mara baada ya mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Congo Brazaville.

Uongozi wa GFA umethibitisha kufanya hatua hiyo kufuatia kushtushwa na maamuzi ya kipa huyo mwenye umri wa miaka 33 ambayo aliyotoa jana mara baada ya mazoezi ya timu ya taifa ambayo inajiandaa na mchezo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika za mwaka 2012.

Sababu kubwa ya Richard Kingson kufanya maamuzi hayo ya kushtukiza ni kufuatia kuchoshwa na vitisho pamoja na lugha za matuzi ambazo amekua akizipata kutoka kwa mashabiki wa soka nchini Ghana ambao mara kwa mara wamekua wakidai huwa anafanya uzembe anapokua langoni.

Kubwa lililomkasirishwa zaidi ni lugha ya matuzi aliyotupiwa jana katika mazoezi ya timu ya taifa yanayoendelea mjini Accra ambapo shabiki mmoja akidiriki kufanya hivyo kufuatai bao alilofungwa katika mazoezi hayo.

Makamu wa raisi wa chama cha soka nchini Fred Pappoe amesema wanaamini mazungumzo yanayoendelea kati yao na Richard Kingson yatafikia muafaka mzuri hatua itakayopelekea kubadili maamuzi yake.

No comments:

Post a Comment