KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, June 1, 2011

Sami Khedira AONYESHA DALILI ZA KUREJEA KAZINI.


Kiungo wa klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania Sami Khedira huenda akawa fit kabla ya mchezo wa mwishoni mwa juma hili wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Ulaya za mwaka 2012 ambao utashuhudia timu ya taifa ya Ujerumani ikipambana vilivyo na timu ya taifa ya Austria.

Sami Khedira anafikiriwa kuwa fit kabla ya mchezo huo kufuatia kuonyesha maendeleo mazuri ya jeraha la paja ambalo lilimsababisha kuukosa mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Uruguay ambao walikubali kichapo cha mabao mawili kwa moja.

Kocha mkuu msaidizi wa timu ya taifa ya Ujerumani Hansi Flick ameeleza kwamba Sami Khedira jana alifanikiwa kufanya mazoezi akiwa pekee yake hatua mbayo wameipokea kwa mikono miwili na kudhani huenda wakamtumia katika sehemu ya michezo ya mwezi huu.

Amesema endapo atakuwa sawa sawa kabla ya siku ya ijumaa atajumuishwa katika kikosi kitakachoikabili timu ya taifa ya Austria na kama itashindikana huenda akatumika katika mchezo wa June 7 ambapo Ujerumani watarejea uwanjani kuukanyaga dhidi ya timu ya taifa ya Azerbaijan.

Hansi Flick pia akathibitisha taarifa za kujiondoa kikosini kwa kiungo wa klabu ya Bayern Munich Bastian Schweinsteiger kufuatia majeraha yanayomkabili.

No comments:

Post a Comment