KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, July 1, 2011

Alexander Doni KUIHAMA AS ROMA?


Majogoo wa jiji Liverpool, bado wnaapewa nafasi kubwa ya kumsajili kipa chaguo la kwanza wa klabu ya AS Roma Alexander Doni.

Kwa mujibu wa wakala wa kipa huyo Ovidio Colucci, amesema mazungumzo ya usajiliw a kipa huyo yalikuwa yameanza kuchukua mkondo wake siku kadhaa zilizopita lakini utaratibu huo ulivunjia baada ya makubaliano binafsi kutokwenda sawa.

Amesema kwa sasa mazungumzo ya usajili wa kipa huyo yameanza kwa mara nyingine tane huku akiaminiwa maafikiano binafsi kati ya Doni dhidi ya viongozi wa klabu ya Liverpool yatakaa sawa.

Hatya hivyo bado mikakati ya kusajiliwa kwa kipa huyo kutoka nchini Brazil inaendelea kuwachanganya mashabiki wa klabu ya Liverpool ambao wanajiuliza ni vipi nafasi ya kipa wa sasa itakavyoendelea kuheshimiwa klabuni hapo?

Pepe Reina amekua akihusishwa na taarifa za kutakakurejea nyumbani kwao Hispania kujiunga na klabu ya Atletico Madrid ambayo tayari imeshamuachia kipa wao David De gea.

Lakini pamoja na kuwepo kwa taarifa hizo Pepe Reina ameendelea kusisitiza kwamba taendelea kusalia Anfield kama mkataba wake unavyoelekeza.

No comments:

Post a Comment