KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, July 4, 2011

NANI KUACHWA KATIKA KIKOSI CHA MENEJA MPYA WA CHELSEA?


Beki wa kiingereza Ashley Cole pamoja na kiungo kutoka nchini ufaransa Florent Malouda wametoa mustakabali wao ndani ya klabu ya chelsea kwa kusema hawatarajii kuondoka katika kipindi hiki licha ya kuhusishwa na taarifa za kuwa mbioni kuondoka huko Stamford Bridge.

Wachezaji hao wawili wamelazimika kuzungumza kauli hiyo ya kubaki jijini London huku wakiamini wapo kwenye mipango ya meneja mpya wa klabu ya Chelsea Andre Villas-Boas alietangazwa kuwa mrithi wa nafasi iliyoachwa wazi na Carlo Michelangello Ancelotti.

Wachezaji hao toka msimu uliopita wamekua wakihusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na klabu ay Real Madrid ya nchini Hispania ambayo ipo chini ya Jose Mourinho ambae kwa sasa anaendelea kufanya usajili ambao anaamini utamsaidia kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Ashley Cole amesema taarifa za kutaka kusajiliwa na klabu ya Real Madrid zimekua zikimfurahisha kama mchezaji ambae anataka mafanikio, lakini bado anaamini mafanikio hayo anaweza kuyapata akiwa na klabu ya Chelsea.

Amesema hakuna mtu ambae hataki kufanya kazi na mtu wa karibu ambae walizoeanza kwa muda mrefu, ila anahisi muda huo wa kuwa sambamba na Mourinho kwa sasa haujafika na kama itawadia atafanya hivyo.

Ashley Cole pia amezipuuza taarifa za kutokuwepo katika mipango ya meneja wa klabu ya chelsea Andre villas Boas, ambapo amesema taarifa hizo hazimtisho zaidi ya kuamini kila meneja anaekwenda Stamford Bridge huwa na mipango ya kumtumia mchezaji anaemkuta klabuni hapo.

Nae Florent Malouda amesema bado ana mkataba na klabu ya chelsea hadi mwaka 2013 na anatamani kuendelea hadi mwaka 2014 kama itawezekana huku akiamini kuendelea kuwepo Stamford Bridge kwa kipindi hicho kutaendeleza mikakati ya kupatikana kwa mafanikio.

No comments:

Post a Comment