
Mshambuliaji kutoka nchini Togo Emmanuel Adebayor amesema bado ana matumaini ya kusajiliwa na klabu ya Real madras ambayo aliitumikia katika sehemu ya msimu uliopita kwa mkopo akitokea Man City.
Emmanuel Adebayor ambae alifanikiwa kufunga mabao mane akiwa na klabu hiyo ya nshini Hispania amesema wakati akiondoka Stantiago Bernabeu, jose Mourinho alimueleza mipango yake ambayo ilimuhakikishia huenda akawepo katika kikosi cha Real Madrid msimu ujao.
Amesema meneja huyo kutoka nchini Uero amejipanga kwa mengi kwa ajili ya kuhakikisha anatimiza malengo ya klabu ya real Madrid ambayo bado ina deni la kurejesha heshima iliyopotea kwa misimu kadhaa sasa licha ya kutwaa ubingwa wa kombe la mfalme msimu uliopita.
Hata hivyo mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, amedai kwamba mbali na Mourinho kumuweka wazi juu ya mipabngo yake, pia wachezaji wa klabu hiyo bado wanaonyeha nia ya kutaka kucheza nae kikosini msimu ujao.
Mpango huo wa Emmanuel Adebayor wa kutaka kubaki nchini Hispania tayari umeshaanza kuingiwa na taarifa za kukatishwa tamaa kufuitia klabu ya Zenit St Petersburg kutangaza hadharani kumuhitaji katika kipindi hiki cha usajili.
No comments:
Post a Comment