KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, July 22, 2011

Alexis Sanchez MAMBO SAFI FC BARCELONA.


Mabingwa wa soka nchini Hispania pamoja na barani ulaya kwa ujumla, Fc Barcelona wameafiki kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Chile pamoja na klabu ya Udinese Alexis Sanchez.
FC Barcelona wamekubalia kufanya uhamisho huo kwa gharama ya euro million 26 ambazo ni sawa na paund million 23 ambazo zimepunguzwa kutoka zaidi ya paund million 30.

Sanchez aliekua nchini argentina sambamba na kikosi cha timu ya taifa ya chile, atafanyiwa vipimo siku za hivi karibuni na endapo atafanikiwa kukidhi vigezo vya kiafya vya wana Catalan atasaini mkataba wa miaka mitano wa kuichezea Barcelona.

Kumalizika kwa usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22, pia kunamaliza zogo kutoka kwenye vilabu kadhaa amvbavyo vilionyesha nia ya kutaka kumsajili hapo awali kabl ya Barcelona kusalia katika utaratibu huo pekee yao.

Klabu zilizotia nia ya kumsajili Sanchez mwishoni mwa msimu uliopita ni Man City, Man Utd pamoja na Real Madrid.

No comments:

Post a Comment