
Kipa kutoka nchini Oman Ali Abdullah Harib Al-Habsi, hatimae amekamilisha ndoto zake za kuihama klabu ya Bolton Wanderers, na kujiunga moja kwa moja na klabu ya Wigan ambayo ilimsajili kwa mkopo msimu uliopita.
Ali Al Habsi ambae amechangia kwa kiasi kikubwa kuibakisha Wigan katika michuano ya ligi kuu nchini Uingereza kufuatai sakata la kuwa karibu kuporomoka daraja msimu uliopita amekamilisha ndoto hizo kwa ada ya uhamisho wa paund million 4.
Kuondoka kwa kipa huyo mwenye umri wa miaka 29, huko Reebok Stadium kumechangiwa na hatua ya kukosekana kwa nafasi katika kikosi cha kwanza cha Bolton ambacho kimekua kikimtegemea sana kipa kutoka nchini Finland Jussi Jaaskelainen.
Owen Coyle meneja wa klabu ya Bolton Wanderers amezungumzia hatua ya kuondoka kwa Ali Al Habsi ambapo amesema bado alikua na nafasi ya kumbakisha kipa huyo kwa vigezo vya kumpatia nafasi ya kucheza kila mara, lakini hana budi kumshukuru kwa mchango wake alioutoa kwa kipindi chote alichokuwepo klabuni hapo na daima ataheshimu maamuzi yake ya kuondoka.
Akiwa na klabu ya Wigan kwa mkataba wa mkopo msimu uliopita Ali Abdullah Harib Al-Habsi amefanikiwa kukaa langoni katika michezo 33.
No comments:
Post a Comment