
Washambuliaji Alexandre Pato pamoja na Neymar ameonyesha kukasirishwa na matokeo ya sare yaliyopatikana katika mchezo wa usiku wa kuamki hii leo ambapo timu ya taifa ya Brazil ilikua ikitupa karata yake ya kwanza kwenye fainali za mataifa ya bara la Amerika ya kusini *Copa America* dhidi ya timu ya taifa ya Venezuela.
Washambliaji hayo wameonyesha hali hiyo, walipozungumza katika mkutano na waandishi wa habari ambapo wamesema, matokeo yaliyopatikana uwanjani hayakuwafurahisha kutokana na kikosi chao kupewa nafasi kubwa ya kushinda.
Wamesema walikua hawana sababu ya kuishindwa kutimiza lengo la kupatikana kwa ushindi na kilicho wagharimu ni kukosekana kwa umakini katika harakati za umaliziaji.
Hata hivyo Alexandre Pato pamoja na Neymar wameahidi kufanya shughuli ya ziada kuhakikisha wanachomoza na ushindi katika mchezo ujao wa kundi la pili ambao utawakutanisha na timu ya taifa ya Paraguay.
Mchezo mwingine wa kundi la pili katika michuano hiyo ulikua kati ya timu ya taifa ya Paraguay dhidi ya Ecuador ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bila kufungana.
Hii leo fainali hizo zinaendelea kwa michezo ya kundi la tatu ambapo timu ya taifa ya Uruguay itashuka dimbani kupambana na Peru na mchezo mwingine utakua kati ya timu ya taifa ya Chile dhidi ya mabingwa wa CONCACAF Mexico.
No comments:
Post a Comment