
Wakati wachezaji wa Arsenal wakitarajia kurejea mazoezini juma hili, beki wa ksuhoto wa klabu hiyo Gael Clichy huenda asiwe miongoni mwa wachezaji hao na pengine akawa katika kundi la kuitumikia Manchester City inayotarajiwa kufanya ziara nchini Marekani pamoja na Canada.
Clichy, mwenye umri wa miaka 25, anahisiwa kutokuwepo katika kundi la wachezaji wa klabu ya Arsenal litakaloanza maandalizi ya msimu ujao wa ligi, baada ya kuonekana mjini Manchester jana jioni huku ikihisiwa huenda yupo mjini humo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya.
Kwa kipindi cha majuma matatu sasa beki huyo wa kushoto amekua katika vita vikali vya kugombewa na baadhi ya vilabu vya soka nchini Uingereza na nje ya nchi hiyom, lakiani inasmeekana Man City wamefanikiwa kumnasa baada ya kukubalia kutoa kisi cha paund million 7 kama ada ya uhamisho wake kutoka kaskazini mwa jiji la London.
Endapo dili la uhamisho wa Gael Clichy litakamilishwa, ataacha kumbu kumbu kwa mashabiki wa wa klabu ya Arsenal ambao wamemshuhudia akiitumikia klabu hiyo kwa muda wa miaka minane iliyopita huku akicheza michezo 187 na kufunga mabao amwili.
Katika hatua nyingine kiungo wa kifaransa Samir Nasri, huenda akawa mchezaji mwingine anaehisiwa kuondoka klabuni hapo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi, baada ya kuendelea kusema ana ukame wa kusaka mataji.
Nasri amesema ukame huo wa kusaka mataji anahitaji kuumaliza akiwa na kikosi cha klabu chenye matamanio ya kufanya hivyo na endapo akatamilisha azma hiyo asichukuliwa vibaya na mashabiki wake wanaompenda.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, anahusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na mabingwa wa soka nchini Uingereza Man Utd pamoja na mahasimu wao Man city.
No comments:
Post a Comment