Kocha mkuu wa kikosi cha timu ya taifa ya Argentina Sergio Batista, hii leo anapewa matumaini makubwa ya kufanya mabadiliko katika kikosi chake ambacho mpaka sasa kimeshindwa kuchomoza na ushindi kwenye michezo miwili ya kundi la kwanza katika fainali za mataifa ya bara la Amerika ya kusini *COPA AMERICA*.
Sergio Batista anapewa matumaini hayo huku kikosi cha Argentina kikitakiwa kusaka ushindi katika mchezo wa hii leo ambao utakuwa wa mwisho katika kundi la kwanza ambao utawakutanisha dhidi ya timu ya taifa ya Costa Rica.
Mabadiliko hayo yanategemea kumpa uhuru Lionel Messi wa kucheza kama anavyokua Barcelona ambapo atasaidiana na Fernando Gago atakaembadili Ever Banega ambae alishindwa kuonyesha makeke katika mchezo uliopita dhidi ya Colombia.

Wachezaji wengine wanaotarajiwa kupewa nafasi hii leo ni Gonzalo Higuain pamoja na Sergio Aguero ambao katika michezo iliyopita wamekua wakiwabadili akina Carlos Tevez pamoja na na Ezequiel Lavezzi.
Kufuatia mabadiliko hayo yanayotarajiwa kufanywa kiksoi cha Argentina kinatazamiwa kuwa na sura ifuatayo ambapo kipa atakua:
Sergio Romero
MABEKI
Pablo Zabaleta, Javier Zanetti, Nicolas Burdisso, Gabriel Milito
VIUNGO
Fernando Gago, Javier Mascherano,
Angel Di Maria; Lionel Messi,
WASHAMBULIAJI
Gonzalo Higuain, Sergio Aguero.
Wakati huo huo gwiji wa soka nchini Argentina, Diego Armando Maradona amemtetea kiungo mshambuliaji Lionel Messi ambae amekua akilalamikiwa kucheza chini ya kiwango katika fainali hizo toka zilipoanza mwanzoni mwa mwezi July.
Diego Armando Maradona amesema kiungo huyo hapaswi kulaumiwa kama ilivyo hivi sasa zaidi ya mashabiki kufahamu kwamba Lionel Messi kwa sasa amechoka kufuatia shughuli kubwa aliyoifanya msimu uliopita akiwa na klabu yake ya Barcelona ambayo ilifanikiwa kucheza mchezo wa fainali wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Man Utd.
Amesema mwishoni mwa juma lililopita alifanya mazungumzo na Messi na alimtaka kuzidisha juhudi binafsi za kufanya vyema uwanjani lakini bado anatambua mchezaji huyo alistahili kupewa muda wa kupumzishwa angalau katika michezo miwili ya mwanzo.

Hata hivyo amemtakia kila la kheri ili aweze kufanya vyema usiku huu ambao una ufunguo maalum wa kuiruhusu Argentina kutinga kwenye hatua ya robo fainali endapo ushindi utapatikana na kama itashindikana, wenyeji hao watakuwa watazamaji.
Mpaka sasa msimamo wa kundi la kwanza waonyesha kwamba timu ya taifa ya Colombia inaongoza kundi hilo kwa kuwa na point saba baada ya kushinda mchezo wao wa jana dhidi ya Bolivia.

No comments:
Post a Comment