
Kiungo mwenye nyota ya kupendwa ulimwenguni David Beckham, anajiandaa kucheza na kikosi cha klabu yake ya zamani ya Man utd ambacho kitafanya ziara nchini humo tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi.

David Beckham, anajiandaa kucheza mchezo huo, baada ya kuchaguliwa na kuwa miongoni mwa wachezaji 11 wanaounda kikosi cha Major League football All-Star ambacho kitashuka dimbani July 27 kupambana na mabingwa hao wa Uongereza kwenye uwanja wa Red Bull Arena uliopo mjini New Jersey.


Katika kikosi hicho kinachoundwa na wachezaji waneocheza ligi kuu ya nchini Marekani pia yupo kiungo mshambuliaji ambae aliwahi kuichezea Everton kwa mkopo Landon Donovan, beki wa zamani wa FC Barcelona Rafael Marquez pamoja na mshambuliaji wa zamani wa klbu ya Arsenal pamoja na Barcelona Thierry Henry.
No comments:
Post a Comment