KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, July 12, 2011

SAMIR NASRI NA SONGOMBINGO LA KUONDOKA EMIRATES.


Meneja wa mabingwa wa soka nchini Uingereza Man Utd Sir Alex Ferguson amesema kiungo wa kifaransa Samir Nasri yu radhi kuondoka Arsenal lakini hana mipango ya kujiunga na kikosi chake kama taarifa zilizoripotiwa siku za hivi karibuni.

Sir Alex Ferguson ameliweka jambo hilo wazi, mara baada ya kuwasili mjini Boston nchini Marekani sambamba na kikosi chake ambacho kitaweka kambi siku kadhaa nchini humo tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi ambao utaanza kati kati ya mwezi August.

Meneja huyo mwenye umri wa miaka 69 amegusia suala hilo alipokuwa akijibu sehemu ya maswali aliyoulizwa na waandishi wa habari ambao walitaka kufahamu ni vipi alivyojipanga kufanya usajili wa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Paul Scholes alietangaza kustahafu soka mwishoni mwa wezi May mwaka huu.

Amesema mipango hiyo inaendelea na alitegemea usajili wa Samir Nasri ungekua sahihi lakini mpaka sasa ameona hakuna dalili zozote za kumpata mchezaji huyo aliesajiliwa na klabu ya Arsenal mwaka 2008 akitokea Olympique de Marseille kwa ada ya uhamisho wa paund million 12.

Wakati Sir Alex Ferguson akionyesha kukata tamaa katika harakati zake za kumsajili Samir Nasri, tayari meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger ameshatoa msimamo wa kuhakikisha anaendelea kumuhodhi mchezaji huyo katika msimu mpya wa ligi.

Wenger alitoa msimamo huo mara baada ya kuwasili mjini Kuala Lumpur nchini Malaysia hapo jana sambamba na kikosi chake ambacho kesho kitashuka dimbani kupambana na kikosi maalum cha nchi hiyo.

Wakati huo huo beki na nahodha wa zamani wa klabu ya Man utd Garry Neville ameupa tano usajili wa wachezaji watatu uliofanywa na Sir Alex Ferguson hadi hivi sasa kwa kusema ni usajili mzuri na anaamini itakisaidia kikosi cha klabu hiyo kutetea vyema taji lake la nchini Uingereza.

Garry Neville amesema mchezaji Ashley Young aliesajiliwa klabuni hapo akitokea Aston Villa ana uzoefu mkubwa, kipa David de Gea nae ana uzoefu wa kucheza michezo ya kimataifa sambamba na beki Philip Anthony Jones alietokea Blackburn Rovers.

No comments:

Post a Comment